Skip to main content
job

MKUFUNZI MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII II – USHONAJI NA UBUNIFU WA MITINDO (TAILORING AND FASHION DESIGN)

Various Government MDAs (via PSRS)

Location
Tanzania
Workplace
Not specified
Engagement
Not specified
Closing date
31 July 2026

About this opportunity

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hii.

Responsibilities

  • Kufundisha masomo ya fani mbalimbali zinazofundishwa katika vyuo.
  • Kutayarisha mpango wa kazi wa mafunzo.
  • Kupima maendeleo ya wanachuo katika nadharia na vitendo.
  • Kutunza vifaa vya kufundishia.
  • Kufanya na kutoa taarifa za utafiti.
  • Kutoa ushauri wa kitaalam.
  • Kuandaa kanuni na taratibu za kusimamia mitihani chuoni.
  • Kutunga na kusahihisha mitihani.
  • Kufanya utafiti utakaosaidia kutoa majibu kwa changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo katika jamii.
  • Kutoa ushauri juu ya kuboresha taaluma chuoni na kuendeleza mafunzo nje ya chuo.

Requirements

  • Wahitimu wa Kidato cha Nne/Sita.
  • Stashahada ya Ushonaji na Ubunifu wa Mitindo (Tailoring and Fashion Design) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Kuambatisha vyeti vya taaluma na nakala za vyeti zilizothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Kuambatisha barua ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.

Eligibility

  • Lazima awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Asizidi umri wa miaka 45.
  • Waajiriwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Benefits or funding

  • Ngazi ya mshahara: TGS C.

Apply on the official source

Ajira Lounge does not collect your application for this listing. Check the destination address before sharing personal information.

Open official application page

Something wrong with this listing?

Report suspected fraud, expired information, or an unsafe application method.