job
MKUFUNZI MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII II – UANDAAJI WA CHAKULA (FOOD PRODUCTION)
Various Government MDAs (via PSRS)
- Location
- Tanzania
- Workplace
- Not specified
- Engagement
- Not specified
- Closing date
- 31 July 2026
About this opportunity
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hii.
Responsibilities
- Kufundisha masomo ya fani mbalimbali zinazofundishwa katika vyuo.
- Kutayarisha mpango wa kazi wa mafunzo.
- Kupima maendeleo ya wanachuo katika nadharia na vitendo.
- Kutunza vifaa vya kufundishia.
- Kufanya na kutoa taarifa za utafiti.
- Kutoa ushauri wa kitaalam.
- Kuandaa kanuni na taratibu za kusimamia mitihani chuoni.
- Kutunga na kusahihisha mitihani.
- Kufanya utafiti utakaosaidia kutoa majibu kwa changamoto mbalimbali.
Requirements
- Wahitimu wa Kidato cha Nne/Sita.
- Stashahada ya Food Production kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Kuambatisha vyeti vya taaluma na nakala za vyeti zilizothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Kuambatisha barua ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.
Eligibility
- Lazima awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Asizidi umri wa miaka 45.
- Waajiriwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Benefits or funding
- Ngazi ya mshahara: TGS C.