job
MKUFUNZI MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII II- MAGARI (MOTOR VEHICLE MECHANICS)
Various Government MDAs (via PSRS)
- Location
- Tanzania
- Workplace
- Not specified
- Engagement
- Not specified
- Closing date
- 31 July 2026
About this opportunity
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hii.
Responsibilities
- Kufundisha masomo ya fani ya Magari katika vyuo.
- Kuandaa mitiririko na mpangilio wa masomo.
- Kusimamia masomo ya vitendo.
- Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi na kwenye mitihani.
- Kufanya utafiti wa mahitaji ya mafunzo katika jamii inayozunguka chuo.
- Kuandaa muhtasari wa masomo.
- Kufanya maandalizi ya namna ya kuendesha mafunzo.
- Kuandaa vielelezo vya kufundishia.
- Kuendesha mafunzo ya nje ya chuo (Outreach Programs).
- Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani.
Requirements
- Wahitimu wa Kidato cha Nne/Sita.
- Stashahada katika fani ya ufundi wa Magari kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Kuambatisha vyeti vya taaluma na nakala za vyeti zilizothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Kuambatisha barua ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.
Eligibility
- Lazima awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Asizidi umri wa miaka 45.
- Waajiriwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wenye kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Benefits or funding
- Ngazi ya mshahara: TGS C.